Habari na taarifa mbalimbali


Habari za shule yetu | Tazama habari nyingine | Go Home | Go to events page


Kufunguliwa shule kwa mwaka mpya wa masomo 2019
Posted on: 2018-12-18 07:01:25
Shule yetu itafunguliwa tena siku ya jumatano ya tarehe 02/01/2019, ambapo wale wa bweni wanatakiwa waje siku moja kabla, ambayo ni tarehe 01/01/2019 kabla ya saa 10:00 jioni. Kwa wale wanafunzi watakaochelewa zaidi ya muda huo waje na wazazi wao. Pia tunawakumbusha wazazi kutimiza wajibu wao wa kulipa ada kwa wakati. UJUMBE KUTOKA OFISI YA MKUU WA SHULE, "Wanafunzi wengi wa kiume wana suruali za sare ya shule ambazo wamezibana chini. Kipimo cha suruali ya sare ya shule ni inchi 16 upana wa chini miguuni. Hivyo, ukiwa kama mzazi au mlezi, unaombwa umuulize mtoto kuhusu suruali yake, kama amerudi nayo ikague kama imebanwa chini miguuni, irekebishe. Kama ikishindikana ujiandae kumnunulia nyingine kwa ajili ya mwaka mpya wa masomo 2019. Kutoka ofisi ya mkuu wa shule".