Matokeo ya Usaili wa tarehe 26-09-2026 | Taratibu za kujiunga kidato cha 1, 2027 (Joining Istructions)

"Education is not a way to escape poverty, it is a way to fight it" - Mwl J. K. Nyerere

Mitaala

 

Asubuhi shule yetu inafuata mitaala iliyotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kidato cha kwanza hadi kidato cha sita),

kwa kuzingatia imani na maadili ya Kanisa Katoliki, pamoja na mila njema za Watanzania ili nchi iweze kujengwa kwa uimara.

Masomo ya Bible Knowledge na Divinity ni ya lazima kwa Wakristo wote.

Aidha, masomo ya Dini yanafundishwa kadiri ya imani ya wanafunzi na utayari wa walimu wa kujitolea kutoka dini husika

Lugha ya Kiingereza ndiyo itakayotumika kufundishia kwa kuzingatia maelekezo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Shule yetu ni ya sekondari kuanzia kidato cha 1 hadi cha 6. Kuanzia mwaka 2010 asubuhi imekuwa na mikondo 24 (6x4) .

 

Shule yetu inapokea hata watu waliochelewa kupata elimu (wanandoa, wafanyakazi n.k.), madarasa 32 yanatumika hata jioni na Jumamosi kwa kozi za haraka kuliko kawaida.

Kwa hiyo, wanafunzi ni zaidi ya 3,000. Karibu nusu wanaishi katika mabweni ya shule, na wengine wanatokea nyumbani.

2018 Form IV graduation ceremony

Watch Video

 

Fr. Rikardo conducting a service the day of the form IV 2018 graduation

Watch Video

 

School scauts performing in front of a guest of honor

Watch Video